Dhamira ya somo tajwa nikukufanya ubadilike katika mtazamo mzima wa kufikiri na kuamua katika maisha yako.
Leo hii mwanafunzi yoyote ambaye anasoma ukimuuliza swali, je, unasoma ili iweje?
Bila shaka majibu ya walio wengi watakwambia, mimi nataka kuwa mwalimu, mwingine anataka kufanya kazi benki au urubani, yote ni sawa! lakini, je, masomo au elimu anayoisoma moja kwa moja inampeleka kuwa rubani, mwalimu, askari, mwandishi, mwanamuziki na fani zingine? Utakuta hamna.
Watu wengi wanaamini baada ya masomo kuna ajira na siyo KUJIAJIRI, wengi wanaamini wakimaliza chuo kwa masomo au mchepuo aliochukua basi atapata kazi fasta lakini kwenye uhalisia wa maisha hauko hivyo.
Bila KUFIKIRIA, KUSOMA AU KUSOMESHA mwanao au mpenzi wako kwa lengo la kuja kujiajiri basi kila siku utaendelea kulalamika kuwa serikali haijatoa ajira mpya.
Binafsi sina elimu kubwa sana ya kuajiriwa ila ninaelimu kubwa zaidi ya kujiajiri.kuna wakati nauchukilia vibaya mfumo mzima wa elimu yetu kwa sababu tu ni kama unampotezea mtu malengo yake, muda na mambo mengine, kwani mwanafunzi anasoma akijua anakuja kuajiriwa.Katika uhalisia hizo ajira ambazo unazifikiria hazipo, na ni ujinga kusoma ukiamini utaajiriwa na kupata maisha mazuri.Kama una mtazamo huo, umeula wa chuya, katika uhalisia wa maisha nje ya shule ni tofauti sana. Kuna kuzunguka na vyeti weeee na kazi hakuna, kuna kuombwa rushwa za pesa au ngono, kuna upungufu wa ajira zenyewe.
Lakini kama mfumo ungekuwa unakuandaa kujiajiri bila shaka kila mtu angekula mazao yake.Fikiria zaidi kuhusu kujiajiri hata kama uko kwenye ajira, pamoja na kwamba haiwezekani wote tukajiajiri lakini wewe ambaye umebahatika kupata fursa ya kujiajiri basi fanya hivyo.
Msomeshe mwanao kwa kile anachokipenda, mtengenezee mazingira ya kujiajiri, kuwa mzalishaji wa bidhaa ili akimaliza masomo yake ajue anachofanya.Kama unasoma, soma kwa kujiajiri na siyo kukalia vimbweta kwa kuamini kuwa unasoma ukaajiriwe.Ninachoamini mabadiliko yanaanza na wewe muhusika kwa kujitambua kisha kufanya yale ambayo unahisi yanastahili kufanywa na wewe au mtu yeyote anayejitambua.
Acha kuifanya akili yako kuwa tegemezi, akili yako kuiegemeza kwenye kuajiriwa. Kwani huwezi kufanya japo jambo dogo la kujiajiri angalau kwa kufungua kibanda cha pipi, machungwa au genge kwa sababu tu una amini una tuzo unayostahili baada yakuhitimu chuo.
Hii siyo nchi ya hivyo, hata huko kwingine ambako unahisi kuna ajira kibao, napo kuna shida kama huku, ila kwa kuwa mfumo wao wameufanya kujiajiri zaidi na si kuajiriwa, ndiyo maana leo hii wametuacha mbali kimaendeleo.
Nadhani kwa hali ya nchi yetu kwa sasa inaonekana kwamba ajira ziko chache sana kwa hivyo kilichopo sahvi ni kukuza akili yako katika kutoitegemea kuajiriwa bali jitengenezee mazingira ya kuwa mbunifu wewe uwe mwajiri ya walio wengi. Hapo nimekusogezea baadhi tuu ya fursa ndogo ambayo mtu unaweza kuvifanya hata ukiwa na mtaji mdogo.
Fursa za ujasiriamali za kujiajiri kwa kutumia mtaji wa kawaida mpaka mtaji mkubwa:
Kufungua studio za kupiga na kusafisha picha, Kufungua yard kwa ajili yakuosha magari.
Kufungua Duka la kuuza nguo mbalimbali; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali Kushona na kuuza nguo Kushona na kukodisha nguo za harusi pamoja na kuuza vipodozi.
Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano ,kudesign Kuuza software mbalimbali ; mfano Antivirus,Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k Website updating/ Database.
Kununua vifaa vya ujenzi kama Mashine za kukoroga zege na kukodisha Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. Kutengeneza na kuuza tofali japo hii inahitaji kidogo kujiweka vizuri katika mtaji naamanisha mtaji uwe mkubwa kidogo.
Kujihusisha na kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo,Mbuzi, Ng’ombe,nguruwe Kuku, Bata, na wengine najua wengi wetu wanaizarau sana kilimo pamoja na ufugaji lakini kilimo kinalipa kutegemea na sehemu kwa hivyo unalinganisha sehemu ambayo wewe unishi na zao ambalo linaweza kustahimili, ufugaji wa kuku ni fursa tosha ya kukutoa wewe kijana. Katika sehemu nyingine nitakuletea namna ambavyo ufugji wa kuku unaweza kujitengeneze kipato kupitia kuku.
Kufungua stationari na cafĂ© mbalimbali,Kusajili namba za simu na kuuza vocha Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA mfumo huu wa mawasiliano unategezeza pesa cha msingi ni kujaribu bila kukata tamaa ndiyo siri ya mjasiriamali. Pia Kuuza ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV,TNG, Digitech,Continental.
Kufungua biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering). Kujenga hostel, kuanzisha nyumba za kupangisha na kuanzisha saluni, kuacha tu mengine saluni unaweza kuendesha kwa hali ya kawaida saluni za kike na za kiumezote hizi zinaweza kukuingizia kipato, aidha kujenga nyumba za kukodisha hizi ni asset ambazo ni za uhakika ambazo mtu unaweza kuvifanya na Zikakuingizia kipato.
No comments:
Post a Comment